
Nyota wa zamani wa Real Madrid, Marcelo Vieira da Silva Júnior almaarufu Marcelo raia wa Brazil ametangaza kustaafu soka la kulipwa akiwa na umri wa miaka 36.
Kupitia kurusa zake za mitandao ya kijamii Marcelo ameandika .“Safari yangu kama mchezaji inaishia hapa lakini bado nina mengi ya kufanya kwenye mpira wa miguu. Asante kwa kila kitu.”
Beki huyo wa kushoto ambaye ameichezea Brazil mechi 58 huku akifunga magoli 6 alirejea kwenye timu yake ya utotoni ya Flamengo ya Brazil mnamo Novemba 2024 baada ya kuzuru barani Ulaya akivitumikia vilabu vya Real Madrid ya Uhispania na Olympiacos ya Uturuki.
Akiwa na Real Madrid Mbrazil huyo alishinda mataji matano ya UEFA Champions League, manne ya Kombe la Dunia la Vilabu na mataji sita ya Ligi Kuu Uhispania akihudumu Real Madrid kwa miaka 16 kabla ya kutimkia Olympiacos mnamo 2023.