Entertainment

Nandy Asema Ana Nyota ya Ajabu Kwenye Muziki wa Bongofleva

Nandy Asema Ana Nyota ya Ajabu Kwenye Muziki wa Bongofleva

Mwanamuziki kutoka Tanzania, Nandy, amejivunia safari yake ya takribani miaka 10 katika tasnia ya muziki wa Bongofleva, akisema kuwa kila wimbo anaouachia unakuwa hit na kupokelewa kwa kishindo na mashabiki.

Kupitia Instastory, Hit maker huyo wa “Sweety” amewashukuru mashabiki wake kwa kumuunga mkono tangu alipoanza rasmi safari yake ya muziki, akisisitiza kuwa bila wao asingefika alipo leo.

Nandy amesema kuwa anahisi ana nyota ya ajabu kwenye muziki, kwani kila mara anapotoa kazi mpya haipiti muda mrefu kabla haijatawala chati na kufurahiwa na mashabiki ndani na nje ya Tanzania.

Ameongeza kuwa safari yake haijakuwa rahisi, lakini kujituma, nidhamu na baraka za Mungu zimemsaidia kudumu kwa muda mrefu huku akiendelea kushikilia nafasi yake kama mmoja wa wasanii wakike wenye ushawishi mkubwa kwenye Bongo Fleva.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *