
Mwanamuziki wa Bongofleva Nandy ametoa hamasa kwa wasanii wa kike nchini Tanzania kutia bidii kwenye kazi zao kwani ni muda wao kuwa vinara kwenye muziki.
Katika ujumbe huo aliouandika kwenye ukurasa wake wa Twitter Nandy amewataja wasanii wenzake wa kike kama Zuchu ,Saraphina, Maua sama & Abby Chams, huku upande wa maoni meneja wa WcB Wasafi Sallam sk akiwataka kufanya wimbo wa pamoja.
“Nadhan ni muda wetu sisi wanawake kuwa Top of the game. Tunapindua meza,” ameandika Nandy Twitter.
Kauli ya Nandy inakuja wiki moja baada ya Zuchu kudai hataki kushindanishwa na wasanii wa kike maana ngoma zake za sasa zinaingia kwenye ligi ya wanaume.
Utakumbuka kwa sasa Nandy, Zuchu na Maua Sama wanawania tuzo za African Muzik Magazine Awards (AFRIMMA) katika kipengele kimoja cha Msanii Bora wa Kike Afrika Mashariki.