Entertainment

Nandy azindua lebo yake ya muziki

Nandy azindua lebo yake ya muziki

Mwanamuziki wa Bongofleva, Nandy ameunza vyema mwaka 2023 kwa kuja kuwapa nafasi watoto wakike.

Kwenye mkao na waandishi wa habari Nandy ametambulisha rasmi Lebo yake mpya ya muziki iitwayo “The African Princess” ambapo ametaja lengo kubwa la lebo hiyo ni kuinua vipaji vya Watoto wa Kike tu.

“Ninayo furaha kubwa kuileta kwenu Rasmi THE AFRICAN PRINCESS LEBEL…! 2023 lebel ambayo itahusisha wanawake tu! Kama tunavo ona industry ya watoto wa kike ni chache sana na uthubutu umekuwa ni mdogo so tunaimani na kuomba the African princess lebel itaongeza wingi wa vipaji vya watoto wa kike waliopo mtaaani wenye ndoto kubwa ya kuwa wanamziki!!…”, Alisema.

Hitmaker huyo wa “Nimekuzoea” amesema lebo hiyo sio tu ya kitanzania bali pia inapania kuwasajili wasanii wengine kutoka mataifa mengine ya Afrika.

“Lakini pia hii lebel SIO ya wa Tanzania tu! Ni lebel ya AFRICA. So tutarajie kuona vipaji mbali mbali kutoka nchi mbali mbali. Ndo mana inaitwa AFRICAN PRINCESS LEBEL!”, Alisema.

Nandy anakuwa mwanamuziki pekee wa kike wa Bongo fleva kuwa na lebo na pia kusimamia wanamuziki wengine wakike.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *