Entertainment

Nandy kumtambulisha msanii wake kesho

Nandy kumtambulisha msanii wake kesho

Staa wa Bongofleva Nandy ametangaza kutambulisha Msanii wake mpya na wa kwanza kwenye lebo yake ya THE AFRICAN PRINCESS.

Nandy amepost picha ya kwanza ya akiwa na Msanii huyo japo hakuonesha sura yake na kuandika “Tarehe 19/1/2023 ndio siku dunia ya mziki itakutambua, nakuombea sana na nakuamini sana na ninaamini Tanzania na dunia nzima iko tayari kukupokea Msanii wetu wa kwanza kwenye label yetu”

“Leo nina furaha sana kama Msanii, lengo nililojiwekea liende kutimia ni hili, ilikuwa ndoto yangu kubwa kuwavuta Vijana wenzangu mkono na wao wafike sehemu waendayo, The African Princess Label itahakikisha inatafatua vipaji popote pale na kuvileta sokoni na mipango yetu ni kuibua vipaji vya Watoto wakike, Yani hii Lebo ni ya watoto wakike tu, mpaka sasa tunaye msanii mmoja tu”

Kwa upande mwingine Nandy amemrejesha Meneja wake wa zamani Moko Biashara kuwa sehemu ya Menejiment yake kama ilivyokuwa mwanzo “Ukimuona Nandy unamuona Moko na Ukimuona Moko unamuona Nandy, Tunaendelea kufanya kazi, atafanya majukumu yake kama alivyokuwa zamani”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *