Entertainment

Nay wa Mitego Amshusha Marioo Youtube Trending Tanzania

Nay wa Mitego Amshusha Marioo Youtube Trending Tanzania

Msanii wa hip hop Nay Wa Mitego amemshua Marioo na wimbo wake wa Oluwa hadi nafasi ya pili baada ya wimbo wake “Tupo Busy” kushika nafasi ya kwanza kwenye orodha ya ngoma kali trending kwenye mtandao wa YouTube nchini Tanzania.

Wimbo huo umevuta hisia za Watanzania wengi kutokana na ujumbe wake mzito unaogusia hali ya kisiasa na kijamii, hasa kampeni inayoendelea ya kuwasusia wasanii wanaodaiwa kuwasaliti wananchi wakati wa uchaguzi wa Oktoba 28 uliokumbwa na utata, kwa kusimama upande wa serikali.

Ndani ya siku mbili pekee tangu kuachiwa kwake, Video ya Tupo Busy imefanikiwa kukusanya zaidi ya views laki tano (500,000+), huku video ya wimbo wa Marioo iliyoshika nafasi ya pili ikiwa na zaidi ya views milioni 2 ndani ya siku tano.

Baada ya kufanikiwa kushika namba moja, Nay Wa Mitego amejitokeza kupitia ukurasa wake wa Instagram na kutoa ujumbe mzito kwa Watanzania, akiwapongeza kwa mshikamano na maamuzi yao ya kususia nyimbo za wasanii aliowaita wasaliti.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *