Gossip

Akothee Awaonya Wanaume Wanaomtaka Kimapenzi

Akothee Awaonya Wanaume Wanaomtaka Kimapenzi

Msanii asiyeishiwa na matukio kila leo, Akothee, amewaonya vikali wanaume wanaojaribu kuonyesha nia ya kuanzisha mahusiano ya kimapenzi naye, akisema wazi kuwa kwa sasa hayuko sokoni wala hana mpango wa kuingia kwenye uhusiano wowote.

Kupitia ujumbe wake uliojaa msimamo Instagram, Akothee amesema hataki kutafutwa kimapenzi na wanaume wasiokuwa na mwelekeo wa maisha au maandalizi ya kifedha. Ameeleza kuwa mapenzi ya kweli hayawezi kuwepo bila msingi wa kifedha.

Akothee, anayejulikana kwa kujiamini na kusema mambo bila kuficha, amesema anajua anachotaka katika maisha na hawezi kuruhusu kuvurugwa na maneno matamu yasiyoambatana na vitendo. Kwa mujibu wake, wanaume wanaomfuata bila uwezo wa kujisimamia kifedha wanapoteza muda wao.

Mwanamama huyo, amesema amejikita zaidi katika kujijenga binafsi na kukuza biashara zake, huku akiwahimiza wanaume kuwekeza kwanza katika maisha yao kabla ya kufikiria mahusiano.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *