
Rapa Ndovu Kuu ametoa ya moyoni kuhusu watu wanafiki ambao mara nyingi huwafuata marafiki zao kwa ajili ya vitu wanavyomiliki katika maisha.
Kupitia insta story yake kwenye mtandao wa Instagram rapa huyo amewataka akina watu sampuli hiyo kuwaamini marafiki zao kwa uhalisia wao wa maisha na sio kwa vitu vya thamani wanavyovimiliki kwa wakati huo.
Mkali huyo wa ngoma ya “Maggie wa nyumbani” amesema maisha ubadilika haraka, hivyo mali ambayo watu wanamiliki kwa sasa huwa inaisha pia.
Hata hivyo hajabainika ni kitu gani kilimpelekea rapa huyo kutoa kauli hiyo ila wajuzi wa mambo kwenye mitandao ya kijamii wanahisi huenda mahusiano ya kimapenzi ya ndovu kuu yameingiwa na ukungu.