Entertainment

“Niko tayari kumuajiri na kumlipa Eric Omondi Kshs.50,000 kwa mwezi” Ringtone Apoko ajigamba

“Niko tayari kumuajiri na kumlipa  Eric Omondi Kshs.50,000 kwa mwezi” Ringtone Apoko ajigamba

Mwanamuziki asiyeishiwa na matukio kila leo Ringtone Apoko ameendelea kumuwashia moto mchekeshaji Eric Omondi baada ya kudai kuwa yuko tayari kumuajiri kama mfanyikazi wake wa nyumbani.

Kwenye mahojiano na The Trend Ringtone amesema atamlipa Omondi shillingi millioni 50,000 kwa mwezi kwa kuwa amekuwa akiigiza kuishi maisha ya kifahari mtandaoni ambayo kwa mujibu wake hawezi kumudu.

Katika hatua nyingine amemtolea uvivu mchekeshaji huyo kwa kusema kuwa hana kipaji cha ucheshi kwani amekuwa akitumia muda wake mwingi kukosoa shughuli za watu ili azungumziwe mtandaoni.

Ringtone Apoko ambaye amekuwa akijinasibu kuwa msanii tajiri nchini Kenya, kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake mpya uitwao “Ombi Langu” akiwa amewashirikisha wasanii wa kundi la Zabron Singers kutoka nchini Tanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *