
Msanii kutoka Uganda Nina Roz amehapa kumsaidia msanii mwenzake Weasel Manizo kuondokana na uraibu wa dawa za kulevya.
Katika mahojiano yake Roz amesema ana uhusiano mzuri na msanii huyo hivyo ana mpango wa kuanza mazungumzo naye ili aweze kuacha kabisa kutumia dawa za kulevya na arudi tena kujishughulisha na masuala ya muziki.
Mrembo huyo amedai vitendo vya Weasel kumnyanyasa kijinsia baby mama wake Sandra inatokana na msanii huyo kutumia mihadarati kupindukia.
Utakumbuka Nina Roz alikuwa muathiriwa wa dawa za kulevya lakini baada ya kupelekewa kwenye kituo cha kurekebisha tabia ya waraibu wa mihadarati aliweza kuacha kutumia dawa hizo na kuamua kuokoka hivyo amekuwa akitumia muda wake mwingi kanisani akihubiri injili.