Entertainment

NINA ROZ AFUNGUKA KUHUSU UTATA UNAOZINGIRA NYIMBO ZAKE

NINA ROZ AFUNGUKA KUHUSU UTATA UNAOZINGIRA NYIMBO ZAKE

Msanii kike kutoka nchini Uganda Nina Roz amethibitisha kwamba ana hakimiliki za nyimbo ambazo alifanya na prodyuza Daddy Andre kabla hajavunja mkataba wake.

Katika mahojiano yake ya hivi karibuni Nina Roz amesema hana deni la mtu kwenye shughuli zake za muziki, hivyo ataendelea kutumbuiza nyimbo zake kwenye shoo zake.

Nyimbo ambazo Daddy Andre na Nina Roz wanagombania ni pamoja na Nagana, Billboard Kipande, Andele, na Enyonta zote zikiwa zimetayarishwa na Daddy Andre chini ya lebo ya muziki ya Blackmarker Records.

Wiki iliyopita Daddy Andre alitishia kumfungulia kesi  Nina Roz kwa madai ya kuvunja mkataba wake bila kufuata sheria stahiki.

Kupitia barua ya kampuni ya mawakili ya  GM Kibirige and Co. Advocates, prodyuza Daddy Andre alidai kwamba Novemba mwaka wa 2021 Nina Roz alisitisha mkataba wake wa miaka 5 ambao alitia sahihi Juni 8 mwaka wa 2020.

Nina Roz hata hivyo alitakiwa amlipe Daddy Dndre shillingi millioni 120 kwa hasara aliyomsababisha na pia asitumie nyimbo alizofanya Daddy Andre kwenye shoo zake la sivyo atamtupa jela.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *