Entertainment

NINCE HENRY AMCHANA GRAVITTY OMUTUJJU KISA KUJIGAMBA KUWA AMEINGIZA PESA NYINGI KUMLIKO MSANII YEYOTE UGANDA

NINCE HENRY AMCHANA GRAVITTY OMUTUJJU KISA KUJIGAMBA KUWA AMEINGIZA PESA NYINGI KUMLIKO MSANII YEYOTE UGANDA

Msanii na mwandishi wa nyimbo kutoka nchini Uganda Nince Henry amemtolea uvivu rapa Gravitty Omutujju mara baada ya rapa huyo kujinasibu kuwa yeye ni moja kati ya wasanii waliopata shows nyingi baada ya uchumi wa nchi ya uganda kufunguliwa.

Katika mahojiano yake na Galaxy FM Nince Henry amesema ameshangazwa na kitendo cha omuttujju kujigamba mitandaoni ambapo amesema  hakutarijia msanii huyo anaweza fanya jambo kama hilo ikizingatiwa kuwa umri wake hamruhusu kujihususha na mambo ya kijinga.

Hitmaker huyo wa “Cinderella” amehoji kuwa baadhi ya wasanii wamepata shows nyingi kutokana na tasnia ya muziki nchini Uganda kufungwa kwa miaka miwili kufuatia janga la Corona, hivyo haoni kitu cha maana ambacho Gravitty Omutujju anajigamba nayo.

Utakumbuka wiki iliyopita rapa Gravitty Omutujju alitangaza kuwa ameingiza pesa nyingi kutokana na shows ambazo amezipata licha ya watu kuubeza muziki wake ambapo alienda mbali na kusema kuwa haoni wasanii wanaodai muziki wao ni mzuri wakipata shows. Jambo hilo lilizua mjadala mzito kwenye mitandao ya kijamii huku kila mtu akitoa maoni tofauti juu ya suala hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *