
Msanii Nince Henry amewatolea uvivu wasanii wote wanaoishi Makindye nchini Uganda kwa tuhuma za kuwadhamini sana waganga wa kienyeji.
Kupitia mitandao yake ya kijamii Nince Henry amesema wasanii wanaoshi eneo hilo wanafanya vitendo vya ushirikina kama njia moja ya kusafisha nyota yao kwenye shughuli zao za muziki.
Nince henry ametoa changamoto kwa wasanii wenzake kutoishi makindye kutokana na kuongezeka kwa visa vya ushirikana miongoni mwa wasanii ambapo ameenda mbali zaidi na kumtaka msanii Spice Diana ahamie maeneo salama kama Ntide.
Utakumbuka Makindye ni eneo ambalo kuna makaazi ya wanamuziki wengi maarufu nchini uganda ambao wanafanya vizuri kimuziki Afrika Mashariki lakini pia ni sehemu ambayo kuna maeneo mengi ya burudani.