
Mwanamuziki wa Kenya anayeishi Marekani Hubert Nakitare maarufuka kama “Nonini” amefungulia mashtaka mwanamitandao Brian Mutinda na kampuni ya kieletroniki ya Syinix.
Hii ni baada ya mwanamitandao huyo kutumia wimbo wake wa “We Kamu” kwenye matangazo ya kibiashara kwenye mitandao ya kijamii bila idhini yake.
Kulingana na shtaka hilo lilofunguliwa katika mahakama ya milimani jijini Nairobi, mshatikiwa ametakiwa kufika binafsi kortini ndani ya siku 15 au akiwa na wakili wake la sivyo hatachukuliwa hatua kali za kisheria.
Utakumbuka mwezi Aprili mwaka huu nonini alitishia kumfungulia mashataka brian mutinda kwa kutumia wimbo wake bila idhini yake ambapo alitoa nafasi ya mazungumzo kati yake na kampuni ya Syinix na Brian Mutinda lakini inaonekana hatua hiyo haikuzaa matunda yoyote.