
Rapper wa Kike kutoka nchini Kenya Noti Flow amefunguka na kudai kwamba hajawahi faidi na mirabaha ya wimbo wake uitwao Foto Moto ambao alimshirikisha Benzema.
Katika mahojiano yake ya hivi karibuni Noti Flow amesema licha ya kuwekeza pesa nyingi kuandaa wimbo wa Foto Moto na hata kuchezwa kwenye vituo vya redio na runinga nchini hajawahi lipwa hata senti moja kutoka kwenye wimbo huo ambao ulipata umaarufu mkubwa nchini mwaka wa 2020.
Mrembo huyo ameilaumu kampuni ya ngoma iliyokuwa ikisimamia kazi zake kwenye mtandao wa youtube kwa kitendo cha kusalia kimya kuhusu hakimiliki ya wimbo wa Foto Moto baada ya mtumiaji mmoja wa youtube kujitokeza na kudai kuwa noti flow na benzema walimuibia mdundo wake na kisha wakaitumia kwenye wimbo wa Foto Moto.
Utakumbuka wimbo wa Foto Moto wake Noti Flow akiwa amemshirikisha Benzema ilitoka mwaka wa 2020 na video yake kwenye mtandao wa youtube ina zaidi ya views millioni 4.5.