
Mwanamuziki wa Bongofleva, Nuh Mziwanda ameshangazwa na kitendo cha baadhi ya wasanii kuachana na Lebo zao za muziki wakati wapo wengi wanaotafuta nafasi hiyo na kuikosa.
Nuh ameenda mbali zaidi na kusema kuwa ameshindwa hata kuachia EP (Extended Playlist) yake kutokana na kukosa usimamizi.
“Mimi Nilitangaza Kuachia EP ila Mpaka sasa ishakua BP kwangu mana Kila mtu Ana Mtu wake βNawaonea huruma sana Mnaotoka kwenye Usimamizi “, Ameandika Instagram.
Hivi karibuni kumekuwa na wimbi la wasanii mbalimbali kuvunja mkataba na lebo zilizokuwa zinawasimamia kwa sababu mbalimbali ambazo nyingi hazijawekwa wazi.