
Staa wa muziki nchini Nyashinski ameingia ubia wa kufanya kazi na chapa (brand) ya Johnnie Walker kama balozi mpya wa kinywa hicho.
Kupitia mitandao yake ya kijamii Hitmaker huyo wa “Properly” ameshindwa kuficha furaha yake kwa kusema kwamba atatumia nafasi hiyo kukitangaza kinywaji hicho nchi nzima
Awali uongozi wa Johnnie Walker ulisema umeamua kumchagua Nyanshinki kuwa balozi wao kutokana na umaarufu na ushawishi wake kwenye jamii ambapo ulidai atatumia nafasi yake ya usanii kukitangaza vyema.