
Msanii mkongwe nchini Nyashinski ameachia rasmi EP yake mpya inayokwenda kwa jina la “THERAPY.
THERAPY EP ambayo ina jumla ya ngoma nne za moto, haina collabo hata moja, kwani ngoma zote Nyashinski kapita nazo mwenyewe.
Ep hiyo ina ngoma kama Night School, Kabla Tudie, Showman,Tunnel Vision na inapatikana kwenye majukwaa yote ya ku-stream muziki duniani.
Nyashinski ambaye amekuwa kimya kwa kipindi cha miezi kumi na moja, ameachia EP hiyo wakati huu yupo kwenye maandalizi ya tamasha lake la Shin City ambalo litafanyika Novemba 26 mwaka huu mjini Eldoret.