Entertainment

NYOTA NDOGO AINGIA UBIA WA KUFANYA KAZI NA KAMPUNI YA JOY MILLERS LIMITED.

NYOTA NDOGO AINGIA UBIA WA KUFANYA KAZI NA KAMPUNI YA JOY MILLERS LIMITED.

Staa wa muziki nchini Nyota Ndogo amelamba dili nono la kuwa balozi wa unga wa ugali wa Raha Premium.

Nyota Ndogo ametengaza habari hiyo njema kwa mashabiki zake kupitia ukurasa wake wa instagram huku akieleza kuwa ana furaha kujiunga na familia ya Raha Premium.

Lakini pia ameishikuru uongozi wa kampuni ya Joy Miller Limited kwa kutambua nguvu yake na kuhamua kumpatia dili hilo ambalo litamjengea heshima.

Nyota Ndogo sasa atatakiwa kutangaza bidhaa za Raha Premium kwa mashabiki zake kupitia mitandao ya kijamii kwa lengo la kuongeza mauzo ya unga hiyo ya ugali.

Hitmaker huyo wa “Watu na Viatu” anajunga na msanii Bahati pamoja mke wake Diana Marua ambao pia waliingia ubia wa kufanya kazi na kampuni ya Joy millers limited mwezi Agosti mwaka huu.

Ikumbukwe nyota ndogo ni mmoja kati ya wasaani ambao wamewekeza kwenye biashara kuuza vyakula na amekuwa akitumia mitandao ya kijamii kutangaza mgahawa wake ambao ameupa jina la Β Nyota Ndogo jikoni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *