Entertainment

Nyota Ndogo akataa zawadi ya bei ghali kutoka kwa mume wake Henning Nielsen

Nyota Ndogo akataa zawadi ya bei ghali kutoka kwa mume wake Henning Nielsen

Mwanamuziki mkongwe nchini Nyota Ndogo amewashangaza mashabiki baada ya kukataa zawadi ya bei ghali kutoka kwa mpenzi wake mwenye asili ya kizungu.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram amesema hana haja na toleo jipya la simu aina ya iphone 14 ambayo  mume wake Henning Nielsen alikuwa amepanga kumzawadi huku akisema kuwa tayari ana simu aina ya iphone 11 ambayo kwa mujibu wake amerithika nayo.

Hitmaker huyo wa ‘Watu na Viatu” amemtaka mume wake kumnunulia shamba na kumjengea hoteli ya kifahari kwani itawasaidia kama kitega uchumi kipindi ambacho mume wake huyo atastaafu.

Hata hivyo mume wake amesisitiza kuwa atamnunulia simu ya iphone 14  huku akiridhia ombi  la kumnunulia shamba na kumjenga hoteli.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *