
Mkali wa muziki wa Hiphop nchini Octopizzo ametangaza ujio wa wimbo wake mpya aliyomshirikisha na lejendari wa muziki Nyashinski
Octopizzo amethibitisha taarifa hiyo njema kwa mashabiki zake Kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kushare picha akiwa na Nyashinski ambapo amewataka mashabiki wakae mkao wa kula kupokea collabo yao ambayo kwa mujibu wake itakuwa moto wa kuotea mbali.
Hitmaker huyo wa ngoma ya “Motivation” hajeweka wazi ni lini hasa ngoma hiyo itaingia sokoni ila itakuwa wimbo wake wa kwanza kufanya na Nyashinski tangu aanze safari yake ya muziki.
Mbali na hayo, Octopizzo ametangaza kuja na ziara ya kimuziki iitwayo live music tour samba na kuachia album mpya ambayo hajataja Siku Rasmi ya kuachia Album hiyo lakini ameweka baadhi ya picha zikimuonesha akiwa kwenye maandalizi ya Album yake Mpya.
Hii inaenda kuwa Album ya 7 kwa mtu mzima Octopizzo, baada ya Fuego” iliyotoka mwaka wa 2021 ikiwa na jumla ya mikwaju 12 ya moto.