Entertainment

Octopizzo Aipeperusha Bendera ya Kenya Grammy 2026

Octopizzo Aipeperusha Bendera ya Kenya Grammy 2026

Msanii wa hip hop kutoka Kenya, Octopizzo, ameweka historia mpya baada ya kutangazwa kuwa miongoni mwa wasanii walioteuliwa kwa hatua ya kujadiliwa katika mchakato wa Tuzo za Grammy za 2026.

Octopizzo amethibitisha habari hiyo njema kupitia ukurasa wake wa Instagram, akieleza kuwa anahisi heshima kubwa kuona kazi zake zikifikia hatua hiyo.

Wimbo wake “Kadi” umechaguliwa kwa vipengele viwili, Song of the Year na Best Global Music Performance, wakati kazi yake nyingine “June 25th” ikichaguliwa kwa Best African Music Performance.

Rapa huyo ameeleza kuwa hatua hiyo ni ushahidi wa namna muziki wa Afrika unavyopata nafasi kwenye jukwaa la kimataifa,huku akiwashukuru wanachama wa jopo la wapiga kura wa Grammy kwa kuthamini kazi kutoka bara hilo.

Hata hivyo Octopizzo amesema kuwa lengo lake ni kupeleka simulizi za Kiafrika hadi kwenye jukwaa la dunia kupitia muziki wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *