Mtangazaji na mchekeshaji maarufu Oga Obinna ameonya wasanii wa Kenya kuhusu kuendesha biashara zao kwa tahadhari, kufuatia tukio ambapo genge la watu wasiojulikana liliharibu duka la pombe linalomilikiwa na msanii Willy Paul.
Kupitia mitandao ya kijamii, Obinna amesisitiza kwamba wasanii wanapaswa kuwa wanyenyekevu na waangalifu wanapoingia katika biashara nje ya muziki ili kuepuka chuki na mashambulizi ya ghafla.
Ameongeza kuwa mafanikio ya msanii yanapaswa kwenda sambamba na busara katika kushughulika na umma, akieleza kuwa dunia ya biashara ni tofauti kabisa na ile ya burudani, hivyo inahitaji umakini na nidhamu zaidi.
Obinna ametoa kauli hiyo mara baada ya Willy Paul kutangaza kuwa amelikarabati upya duka lake la Pozze Liquor store lilovamiwa na wahuni na kababisha hasara ya mamilioni ya fedha.