Entertainment

Oga Obinna Atokwa na Machozi kwenye Mazishi ya Kimani Mbugua

Oga Obinna Atokwa na Machozi kwenye Mazishi ya Kimani Mbugua

Mtangazaji Oga Obinna amejipata akitokwa na machozi ya uchungu wakati wa mazishi ya mwanahabari Kimani Mbugua, tukio lililofanyika katika eneo la Maragua, Kaunti ya Murang’a.

Katika hotuba yake, Obinna ameelezea maumivu makubwa aliyoyahisi kutokana na kumpoteza rafiki katika tasnia ya habari, akisema wanahabari na wasanii wengi wanapitia changamoto kubwa za kimaisha na kisaikolojia ambazo mara nyingi hawawezi kuzungumzia hadharani.

Ameeleza kuwa tasnia ya habari na burudani imejaa mashindano, presha na upweke unaowafanya wengi kukosa msaada wa kihisia. Amehimiza mastaa kusaidiana na kuinua kila mmoja badala ya kuendeleza mashindano na chuki zisizo na maana.

Obinna pia amewakumbusha mashabiki kwamba maisha halisi ni tofauti kabisa na yanayoonekana kwenye mitandao ya kijamii, akibainisha kuwa mitandao hiyo mara nyingi huficha maumivu na mapambano ambayo watu hupitia kimya kimya.

Mazishi ya Kimani Mbugua, aliyewahi kuwa mtangazaji mwenye kipaji kikubwa, yalihudhuriwa na watu wengi kutoka sekta ya habari na burudani nchini. Wengi walimkumbuka kama kijana mwenye ndoto kubwa, ubunifu na moyo wa kujituma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *