Entertainment

Okello Max Aachia Albamu Mpya “Healing” Yenye Nyimbo 15

Okello Max Aachia Albamu Mpya “Healing” Yenye Nyimbo 15

Msanii maarufu wa muziki wa Kenya, Okello Max, ameachia rasmi albamu yake mpya inayokwenda kwa jina “Healing”, yenye jumla ya nyimbo 15. Albamu hiyo inajumuisha ushirikiano na wasanii mbalimbali maarufu wakiwemo Watendawili, Breeder LW, Vijana Baru Baru, Christin Bella kutoka Tanzania, pamoja na Mordecai Dexx.

“Healing” inaelezwa kuwa mradi wa kipekee unaogusa maisha na mapenzi, huku Okello Max akionyesha ustadi wake wa uandishi wa mashairi, utofauti wa midundo, na ushirikiano wenye nguvu kutoka kwa wasanii wa kizazi kipya.

Katika kusherehekea uzinduzi wa albamu hiyo, Okello Max atafanya tamasha maalum la kusikiliza albamu hiyo (album launch party) tarehe 12 Julai katika ukumbi wa Mass House. Hafla hiyo inatarajiwa kuvutia mashabiki, wadau wa muziki, na wasanii wenzake kwa ajili ya kusikiliza kwa mara ya kwanza nyimbo zote 15, pamoja na burudani ya moja kwa moja.

Uzinduzi wa “Healing” unaonesha hatua mpya katika safari ya muziki ya Okello Max, ambaye anazidi kujikuza kama mmoja wa wasanii wabunifu na wenye ushawishi mkubwa katika tasnia ya muziki wa Afrika Mashariki. Mashabiki wake sasa wanatarajia kuona albamu hiyo ikifanya vizuri kwenye majukwaa ya muziki ndani na nje ya nchi.