Entertainment

Okello Max aachia rasmi Album yake mpya

Okello Max aachia rasmi Album yake mpya

Mwanamuziki kutoka Kenya Okello Max ameachia rasmi Album yake mpya iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki zake.

Album hiyo inakwenda kwa jina la Boss ina jumla ya nyimbo 15 na bonus track moja ambapo amewashirikisha wakali kama Bassman, Bonysun, Suzanna Owiyo, Femi One, Bien Bensoul, Coster Ojwang’, Jocelina, Charisma na Watendawili.

Boss Album  ina nyimbo kama  Pull Up, Nipe Nafasi, Kuwa na Wewe, Kungfu,Boss Oreo na nyingine nyingi.

Boss ni Album ya kwanza kwa mtu mzima Okello Max  tangu aanze safari yake ya muziki  na inapatikana exclusive kupitia mtandao wa kupakua na kusikiliza muziki wa BoomPlay.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *