LifeStyle

Okello Max Akiri Kudanganya Kuhusu Kuwa na Watoto

Okello Max Akiri Kudanganya Kuhusu Kuwa na Watoto

Msanii wa R&B na Afrobeat kutoka Kenya, Okello Max, amekiri kudanganya kuhusu kuwa na watoto, jambo ambalo kwa muda mrefu limekuwa likiwachanganya mashabiki wake.

Katika mahojiano na mtangazaji Shiksha, Okello Max amefafanua kuwa watoto waliowahi kuonekana naye mara kwa mara si wake, bali ni ndugu wa mchumba wake.

Hitmaker huyo wa Taya, ameeleza kuwa shinikizo la mara kwa mara kutoka kwa mashabiki na jamii lilimfanya kuamua kudanganya na kudai watoto hao ni wake, jambo ambalo sasa amelikiri halikuwa sahihi.

Hata hivyo, msanii huyo amebainisha kuwa sasa ameamua kufunguka ili kuondoa dhana potofu na kuweka mambo wazi kwa mashabiki wake. Amesisitiza kuwa uongo huo ulikuwa matokeo ya shinikizo na si sehemu ya maisha yake halisi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *