
Nyota wa muziki Otile Brown ameingia kwenye headline katika mitandao ya kijamii mara baada ya kudai kuwa Mbosso ameiiba idea ya wimbo wake na kuitumia kwenye wimbo wake mpya uitwao”For You Love” ambao amemshirikisha Zuchu.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Otile Brown amedai kwamba Mbosso na Zuchu waliiba mdundo wa wimbo wake uitwao “Baby Love” na kuutumia kwenye wimbo wao bila ridhaa yake.
Hitmaker huyo wa βJerahaβ amedai kwamba angekuwa na roho mbaya angeweza kuiripoti ngoma hiyo kwa Youtube kama njia ya kudai hakimiliki.
Suala hilo limeibua maswali mengi miongoni mwa wadau wa muziki nchini ambao wameenda mbali zaidi na kuhoji kuwa Otile Brown anataka kutumia jina la Mbosso na Zuchu kujitafutia umaarufu.