
Nyota wa muziki Otile Brown anazidi kujikita kileleni kwenye mtandao wa YouTube ambapo kwa sasa amefikisha idadi ya subscribers Milioni 1 kwenye mtandao huo.
Hii inamfanya Hitmaker huyo wa “Jeraha” kuendelea kukaa kileleni kama msanii anayeongoza kwa idadi kubwa ya subscribers kwenye Mtandao wa Youtube kwa wasanii wa Kenya.
Sanjari na hilo, Mkurugenzi wa lebo ya muziki ya Just in Love na hadi sasa Kupitia channel yake ya YouTube kazi zake zimetazamwa zaidi ya mara milioni 251 tangu ilipofunguliwa rasmi Aprili 20 mwaka 2016.
Wasanii wengine kutoka Kenya ambao wapo mbioni kufikisha subscribers millioni moja kwenye mtandao wa youtube ni pamoja na Bahati ambaye ana subscribers laki 9, na Sauti sol ambao wana subscribers laki 8