
Nyota wa muziki nchini, Otile Brown amedai kuibiwa laptop zake mbili aina ya MacBook akiwa kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
Kupitia insta story yake Otile ambaye ametua nchini Tanzania asubuhi ya leo kwa ajili ya shughuli zake za kimuziki ameeleza kuwa walinzi pamoja na watoa huduma walikataa kumpa ushirikiano ikiwa ni pamoja na kuchunguza tukio zima kupitia kamera za CCTV zilizopo eneo hilo.
“”So kwenye airport ya Julius Nyerere nimeibiwa Mac/laptop mbili ila walinzi na watoa huduma wamekataa kutusaidia ndani ya masaa 3 wamekataa kuchunguza kwenye cctv … longest night of my life.Tumetoa hadi report ya police ambayo ndio utaratibu lakini wakakataa… nimeumia sana,” Ameandika.
Hata hivyo hakufichua thamani ya vifaa vyake vya kielektroniki ambavyo vimetoweka katika uwanja wa ndege.