
Msanii nyota nchini Otile Brown ameamua kuzitumia ipasavyo pesa anazozikeshea na kuzitolea jasho.
Hii ni baada ya kutumia kiasi cha shillingi elfu 80 za Kenya kununua viatu aina Balenciaga Crocs boots kama zawadi ya kumbukizi ya kuzaliwa kwake Machi 21 mwaka 2022.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Hitmaker huyo wa ngoma ya “Fed Up” amechapisha video akionekana akizitoa viatu hivyo kwenye boksi huku akiwashukuru mashabiki zake kwa kusapoti muziki wake na kumfanya kuwa namba moja kwenye kiwanda cha muziki nchini..
Otile Brown ambaye kwa sasa yupo nchini Afrika Kusini kwa ajili kusherekea birthday yake anaungana na rapa Kanye West kutoka Marekani ambaye hupendelea kuvaa viatu aina ya Balenciaga Crocs Boots