Mwanamuziki nyota wa R&B nchini, Otile Brown, ameamua kuwapa wanawake maua yao kwa jitihada zao za urembo, akisema sasa anaelewa ni kwa nini kuwa mwanamke ni jambo la gharama kubwa.
Kupitia instastory yake, Otile ameeleza kuwa katika kipindi cha chini ya mwezi mmoja amelazimika kusuka nywele mara tatu, jambo lililomfanya kutambua changamoto za kifedha ambazo wanawake hukumbana nazo mara kwa mara wanapojitunza.
Staa huyo wa “Not For Me” amesema kuwa gharama za kusuka nywele, pamoja na mahitaji mengine ya urembo, ni kikwazo kikubwa ambacho wanawake wengi hulazimika kubeba kila wakati.
Kauli hiyo imezua mjadala, mashabiki wake wakimtania huku wengine wakimpongeza kwa kuonyesha uelewa wa upande wa pili wa maisha ya wanawake.