
Imekuwa kawaida sasa kwa mastaa Duniani kumwaga mamilioni ya pesa hasa kwenye vito vya thamani, magari pamoja na majumba ya kifahari
Staa wa muziki nchini Otile Brown ameamua kuzitumia ipasavyo pesa anazozikeshea na kuzitolea jasho.
Mkali huyo wa “Rup Up” ametumia kiasi cha zaidi ya shillingi milioni 485,000 za Kenya kununua Suitcase aina ya Louis Vuiton.
Hii ni kwa mujibu wa picha ambazo alizishare kwenye ukurasa wake wa Instagram ikimuonyesha akitua nchini akitokea Afrika Kusini ambako amekuwa vacations kwa wiki mbili sasa.
Hii ni mara ya pili kwa mtu mzima Otile BROWN kununua vitu ya thamani kubwa. Mwezi Machi mwaka huu alinunua pia viatu aina Balenciaga Crocs boots kama zawadi ya kumbukizi ya kuzaliwa kwake iliyomgharimu kiasi cha shillingi elfu 80 za Kenya.