
Msanii kutoka nchini Kenya Otile Brown tayari amepata laptop zake mbili zilizoibiwa alipotua nchini Tanzania siku ya jana.
Kupitia video aliyochapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram Otile amethibitisha kupokea laptops hizo aina Mac Book ambayo alizipoteza katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere
Meneja wa msanii huyo Reginald Noriega amefichua kwamba walifanya uchunguzi walifanikiwa kuzipata kompyuta hizo eneo la kinondoni viungani mwa Jijini Dar es Salaam.
Kauli ya Otile Brown imekuja mara baada ya kutoa ahadi ya kuwalipa watakaomrejesha laptops hizo kutokana na stakabadhi zake muhimu ambazo zilikuwa ndani.