
Mwanamuziki maarufu nchini Otile Brown ameshindwa kuendelea kuficha hisia zake za ndani juu ya mapenzi aliyonayo kwa staa wa muziki wa Rnb kutoka Marekani, Toni Michele Braxton.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Otile ameweka wazi hisia zake kwa Michele Braxton kwa kudai kwamba amekuwa akimzimia kimapenzi mwanamuziki huyo kwa muda mrefu na bado anaendelea kuhusudu penzi lake.
“Still crushing on her,” Otile ameandika.
Hitmaker huyo wa ngoma ya Jeraha ameenda mbali zaidi na kumpa maua yake mwanamama huyo mwenye umri wa miaka 54 kwa kusema kwamba ni moja kati ya wanawake warembo zaidi duniani ambao wapo hai.
“One of the sexiest women God ever created,” Amesisitiza.
Hata hivyo mashabiki wametoa hisia mbali mbali kuhusiana kauli hiyo ya Otile Brown huku wengi wakisema wameumizwa na kitendo cha msanii huyo kumzimia kimapenzi mtu mwingine licha ya kuwa wamekuwa wakimtamani kimapenzi.
Utakumbuka Braxton ambaye anatajwa kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na Rapa Birdman amejaliwa kuwapata watoto wawili ambao ni, Diezel Ky Braxton na Denim Cole.