Entertainment

Otile Brown Atangaza Wimbo wa Kumbukumbu kwa Baba Raila Odinga

Otile Brown Atangaza Wimbo wa Kumbukumbu kwa Baba Raila Odinga

Staa wa muziki wa Bongo RnB, Otile Brown, ametangaza ujio wa wimbo mpya wa kumbukumbu kwa Baba Raila Odinga, siku chache tu baada ya kiongozi huyo kuzikwa.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Otile amesema kuwa mwezi Novemba atatoa wimbo ulio karibu sana na moyo wake, akisema ni wimbo wa heshima na kumbukumbu kwa Raila na kwa wote waliopoteza wapendwa wao.

Msanii huyo amesisitiza kuwa baadhi ya matukio ni zenye nguvu kiasi kwamba haziwezi kunyamaziwa, na kwamba muziki wake utakuwa njia ya kuenzi maisha na urithi wa Baba.

Mashabiki wengi wamepongeza hatua ya Otile Brown wakisema ni njia ya heshima na kumbukumbu kwa kiongozi ambaye amegusa maisha ya Wakenya wengi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *