
Staa wa muziki nchini Otile Brown ameonesha kuwa na moyo wa shukrani baada ya kutoa Msaada kwa wakaazi Mikindani, Mombasa.
Otile Brown ambaye alizaliwa na kukulia Mikindani ametoa msaada wa vyakula ikiwemo unga,mafuta ya kupikia na mahitaji mengine ya msingi.
Hitmaker huyo wa ngoma ya “Run Up” ameeleza nia ya kufanya hivyo ni kurudisha fadhila kwa jamii kutokana na mchango mkubwa alioupata kupitia muziki wake.
Hata hivyo wakaazi wa Mikindani wameonekana kumshuruku mwanamuziki huyo kwa moyo ukarimu wa kurudisha mkono kwa jamii.