
Mwanamuziki nyota nchini Otile Brown amewatolea uvivu baadhi ya mashabiki wanaozidi kumkosoa baada ya kuacha kuimba nyimbo zake kwa lugha ya Kiswahili na kugeukia Kiingereza.
Kupitia mfululizo wa insta stories kwenye ukurasa wake wa Instagram, Otile amewataka wanaopinga juhudi zake za kuupeleka muziki wake kimataifa kuanza kujifunza kuhusu mitindo mbali mbali ya muziki huku akienda mbali zaidi na kudai kuwa ataendelea kutoa muziki mzuri kwa lugha ya Kiingereza kwani hatotishwa na maneno ya watu mtandaoni.
“Fk the humble shit for a sec … do y’all even to pay to my kizungu songs au kisa mnapenda Kiswahili mnaboeka ata before y’all give it a chance … mimi ukinipa nafasi nakalisha Africa nzima na dunia kwa ujumla kwani ni Siri”, Aliandika
Katika hatua nyingine, Hitmaker huyo wa ngoma ya “Celebration” amesema kuwa hana muda wa kuuthibitisha ulimwengu mafanikio yake kisanaa kwa kuwa ana kipaji cha kipekee kwenye tasnia ya muziki barani Afrika na kote duniani.
“Na by the way nyimbo za Kiswahili kwangu hamuezi kumaliza msion … sihitaji kuprove chochote uwezo wangu mnaujua … sitochoka kufanya kufanya nyimbo za kimataifa kisa woga … find taste …” Alisisitiza