Entertainment

OTILE BROWN AWAKINGIA KIFUA WASANII WA KENYA

OTILE BROWN AWAKINGIA KIFUA WASANII WA KENYA

Staa wa muziki nchini Otile Brown amewajibu baadhi ya watu wanaowakosoa wasanii wa Kenya wakidai kuwa wamefulia kiuchumi.

Kupitia Instagram Otile Brown amewakingia kifua wasanii wa Kenya kwa kusema kwamba wana mafanikio makubwa kiuchumi Barani Afrika kuliko wasanii wanaozungumzia sana kwenye vyombo vya habari.

Hitmaker huyo wa ngoma ya “Run Up” amewatolea uvivu wadau muziki nchini akisema kwamba wameshindwa na biashara ya muziki na badala yake wamegeukia kuwatupia lawama wasanii wakenya ambao wanaendelea kutia bidii kupitia kazi zao kila uchao.

Utakumbuka Otile Brown amekuwa akiwatetea wasanii wa kenya pindi wanapokosolewa kwenye muziki wao lakini pia amekuwa akiwahimiza wakenya kuunga mkono wasanii wao badala ya kuwasapoti wasanii wa nje.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *