
Staa wa muziki nchini Kenya Otile Brown ametoa rai kwa mashabiki zake wa Tanzania kumrejeshea kompyuta zake mbili za mkononi zilizopotea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
Kupitia instagram live amesema yupo radhi kutoa kiasi chochote fedha kwa mtu yeyote atakayemrejeshea laptop hizo kwani zimemkosesha usingizi.
Aidha ameahidi kuwa hana mpango wa kufungulia mashtaka mtu yeyote atakajitokeza kumrudishia kompyuta zake aina MacBook kutokana na uhitaji wa stakabadhi zake muhimu zilizomo ndani.