Entertainment

Otile Brown Awataka Mashabiki Kumsaidia Kumtafuta Mrembo

Otile Brown Awataka Mashabiki Kumsaidia Kumtafuta Mrembo

Penzi la mjaka mfine, mrembo aliyekutana na Otile Brown katika tamasha la Luo Festival limemkosesha usingizi staa huyo wa R&B. Msanii huyo amekiri waziwazi kwamba alitekwa na mvuto wa mrembo huyo, akidai macho yake na uwepo wake vilimchanganya.

Otile Brown, ambaye mara nyingi huweka wazi hisia zake kupitia muziki, safari hii hakuweza kujizuia bali aliamua kutafuta msaada wa mashabiki wake. Kupitia ukurasa wake wa mtandaoni, aliposti picha yake na mrembo huyo wakiwa karibu, akionekana akimnong’oneza kwa upole kana kwamba macho yake yamefungwa na mvuto wa mrembo huyo.

Staa huyo wa Dusuma hakuishia hapo, alienda mbali zaidi na kuwaomba mashabiki wake wamfikishie ujumbe mrembo huyo kwa kumtag, ishara kuwa hamtaki kumwachia apotee hivihivi.

Mashabiki wake walichangamkia ombi hilo kwa utani na mzaha, huku wengine wakidai huenda Otile anaanza ukurasa mpya wa mapenzi. Kwa upande mwingine, wapo waliotaja tukio hilo kama kiki ya kuitangaza single yake mpya inayokwenda kwa jina la “Not For Me”

Kwa sasa macho yote yameelekezwa kwa mjaka mfine huyo, huku mashabiki wakingoja kuona kama utamu wa tamasha la Luo Festival unaweza kugeuka kuwa simulizi jipya la mapenzi kwa Otile Brown.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *