Entertainment

Pallaso Ageukia Muziki wa Mapinduzi Kuunga Mkono Mabadiliko Nchini Uganda

Pallaso Ageukia Muziki wa Mapinduzi Kuunga Mkono Mabadiliko Nchini Uganda

Msanii wa muziki nchini Uganda, Pallaso, amejiunga rasmi na safu ya wasanii wanaotumia sanaa kuhimiza mabadiliko ya kijamii na kisiasa, baada ya kugeukia muziki wa mapinduzi unaochochewa na harakati za kudai haki na uongozi bora nchini humo.

Pallaso anaeleza kuwa amegeukia muziki wa mapinduzi ili kuwaamsha raia na kuwapa nguvu kudai haki, maendeleo na taifa lenye usawa. Anasema kuwa kuna mambo mengi yanayoendelea nchini, lakini baadhi ya watu wamepuuza hali halisi, jambo linalomchochea kutumia muziki kama chombo cha kuelimisha na kuhamasisha jamii.

Kwa mujibu wa Pallaso, muziki wa mapinduzi unalenga kutoa motisha na matumaini kwa wananchi wanaopitia changamoto, hasa katika kipindi hiki cha kisiasa.

Hata hivyo amesema kuwa ni wakati wa kuchukua hatua kwa sababu mustakabali wa taifa unategemea mabadiliko, akiwahimiza wananchi wa Uganda kudai maisha bora bila uwoga wowote.

Pallaso, ambaye hivi karibuni amerudi ndani ya chama cha National Unity Platform (NUP) kinachoongozwa na Bobi Wine baada ya kujitenga na upande wa chama tawala NRM, amekuwa akihudhuria na kutumbuiza katika mikutano kadhaa ya kisiasa ya NUP kote nchini Uganda.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *