Entertainment

PALLASO AGUSWA NA MASAIBU YA EDDY DEE, AMLIPIA KODI YA STUDIO

PALLASO AGUSWA NA MASAIBU YA EDDY DEE, AMLIPIA KODI YA STUDIO

Mwanamuziki kutoka Uganda Pallaso ameamua kuwa na moyo wa ukarimu kwa aliyekuwa prodyuza wake Eddy Dee.

Msanii huyo ametoa shillingi millioni moja za Uganda kwa prodyuza huyo ili aweze kukamilisha deni la kodi analodaiwa la shillingi millioni 4.

Eddy Dee ambaye amehusika pakubwa kutayarisha nyimbo za pallaso ameweka wazi taarifa hiyo kwa mashabiki zake kupitia mitandao yake ya kijamii ambapo amemwagia sifa mwimbaji huyo kwa kuwa na moyo wa kusaidia.

Hata hivyo masaibu ya prodyuza huyo hajaisha kwa kuwa bado mwenye nyumba anasisitiza kwamba atamruhusu kwenye mjengo wake atapokamilisha pesi zote za kodi.

Utakumbuka juzi kati prodyuza Eddy Dee alifungiwa studio yake baada ya kukosa kulipa kodi kwa takriban miezi 7 ambapo alienda mbali zaidi na kutoa wito kwa wasanii wote aliofanya nao kazi kipindi cha nyuma wamsaidie kulipa kodi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *