Entertainment

Pallaso arejesha akaunti yake ya Facebook kutoka kwa wadukuzi

Pallaso arejesha akaunti yake ya Facebook kutoka kwa wadukuzi

Staa wa muziki kutoka Uganda Pallaso amefanikiwa kurejesha akaunti ya Facebook kutoka kwa wadukuzi.

kupitia ukurasa wake wa Insagram Pallaso ameshindwa kuficha furaha yake kwa kuupongeza uongozi wake kwa kumsaidia kuirejesha chaneli yake ya youtube yenye subscribers laki saba.

“Ni mwaka mmoja na nusu tangu nipoteze ukurasa wangu wa Facebook. Asante Mungu, imerudi,” inasomeka sehemu ya ujumbe ambayo Pallaso amechapisha kwenye Instastory yake.

Kaunti hiyo hajakuwa hewani kwa kipindi cha miezi 18 baada ya kudukuliwa na watu wasiojulikana.

Hata hivyo amewataka mashabiki kuwa makini na matapeli wanaoweza kutumia jina lake kuwalaghai.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *