Gossip

Parroty Afufua Bifu na Toxic Lyrikali Kupitia Picha ya Siri

Parroty Afufua Bifu na Toxic Lyrikali Kupitia Picha ya Siri

Msanii wa muziki wa gengetone, Parroty Vunulu, amezua gumzo mitandaoni baada ya kuwaomba mashabiki wake kumsaidia kutambua picha ya mwanaume asiyejulikana ambaye amekuwa akijitokeza mara kwa mara kwenye sehemu ya maoni ya mitandao yake ya kijamii.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Parroty aliahidi kumpa zawadi ya KSh 1,000 shabiki atakayefanikisha kumtambua mwanaume huyo. Ingawa hakumtaja moja kwa moja, mashabiki wengi wamehusisha picha hiyo na rapa Toxic Lyric Kali, anayejulikana kwa wimbo Backbencher.

Inadaiwa kuwa Parroty na Toxic Lyric Likali hawako kwenye uhusiano mzuri baada ya madai kwamba rapa huyo alimuaibisha Parroty mtandaoni alipomwomba kufanya kolabo. Tukio hili limeendeleza mvutano wa chini kwa chini kati ya wasanii hao, huku mashabiki wakisubiri kuona kama Toxic Lyrikali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *