Gossip

Patello Afunguka Kuhusu Video ya Mkewe Dee Akimpiga Kofi

Patello Afunguka Kuhusu Video ya Mkewe Dee Akimpiga Kofi

Msanii wa muziki kutoka Kenya VJ Patello amevunja ukimya baada ya kusambaa kwa video mtandaoni ikimuonyesha akipigwa kofi na mkewe, Dee, tukio ambalo lilizua mjadala mkali miongoni mwa mashabiki.

Akipiga stori na 2Mbili, Patello ameeleza kuwa kilichoshuhudiwa kwenye video hakikuwa ugomvi, bali ni tukio lililotokea wakati hakuwa na hamasa ya kutumbuiza. Amesema mkewe alikuwa akijaribu kumtia moyo ili achangamke na kuendeleza burudani kwa mashabiki.

Hata hivyo, Patello amesisitiza kuwa hana tatizo na mkewe na kwamba wawili hao wanaendelea vizuri, akiwataka mashabiki wasichukulie video hiyo kwa mtazamo hasi.

Kauli hiyo imeibua mitazamo tofauti miongoni mwa mashabiki. Baadhi wanamtetea Dee wakisema alifanya hivyo kwa nia ya kumtia moyo mumewe, huku wengine wakihisi kitendo hicho kilikuwa cha kudhalilisha msanii huyo mbele ya mashabiki wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *