
Mwimbaji nyota wa muziki kutoka Nigeria, Patoranking ambaye kwa sasa anafanya vizuri na smash hit yake Kolokolo akiwa na Diamond Platnumz, anatajwa kuwa atatumbuiza kwenye Kombe La Dunia 2022 huko Qatar mwezi huu katika tamasha la FIFA Fan tarehe 28.
Tamasha hilo linatarajiwa kufanyika katika uwanja wa Albidda Park wakati wa siku 29 za mashindano ya Kombe la Dunia na halina kiingilio.
Fahamu, michuano ya Kombe la Dunia 2022 huko Qatar inatarajiwa kuanza Novemba 20 na kufikia tamati Disemba 18. Mataifa 32 yatashuka uwanjani kusaka ubingwa wa michuano hiyo mikubwa ya soka duniani.