Sports news

Pele kuagwa jumatatu nchini Brazil

Pele kuagwa jumatatu nchini Brazil

Taifa la Brazil limeanza rasmi siku tatu za maombolezo kufuatia kifo cha nguli wa soka nchini humo, Edson Arantes do Nascimento maarufu Pelé aliyefariki jana Alhamisi baada ya kuugua saratani kwa muda mrefu.

Shughuli ya kuuaga mwili wa marehemu itafanyika Jumatatu ijayo kwa saa 24 katikati ya uwanja wa Santos, ambako ndiyo klabu ya Pelé ya nyumbani alipoanzia kucheza soka akiwa kijana mdogo.

Mazishi ya nguli huyo wa soka yanatarajiwa kufanyika kwenye Ukumbusho wa Necrópole Ecumênica, kaburi la wima huko Santos, ambako aliishi zaidi wakati wa uhai wake. Familia pekee ndiyo inatajwa itahudhuria mazishi hayo.

Watu mbalimbali kutoka pande zote za Dunia wameendelea kutuma salamu zao za heshima na rambirambi kufuatia kifo cha nguli huyo wa soka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *