
Rapper Kanye West (YE) na mpenzi wake mpya Chaney Jones wameachana.
Tovuti ya TMZ imethibitisha taarifa hiyo kwa kusema kwamba wawili hao wamefikia ukomo wa penzi lao baada ya ziara ndefu nchini Japan.
Hakuna taarifa za yupi aliyempiga chini mwenzie lakini taarifa hizi zinakuja ikiwa ni siku chache baada ya kuonekana picha ya Kanye West akicheki movie na mwanamke mwingine.
Kanye West (YE) na Chaney walianza kuonekana hadharani mwezi Februari mwaka huu na tayari mwanadada huyo alishachora Tattoo yenye jina ‘YE’ mkononi.