Entertainment

PENZI LA NOTI FLOW NA KING ALAMI LAFUFUKA TENA

PENZI LA NOTI FLOW NA KING ALAMI LAFUFUKA TENA

Waswali wanasema Penzi ni kikohozi na halifichiki msemo huo umethibitishwa na mwanamuziki Noti flow  mara baada ya kuandika ujumbe ambao umetafisiriwa na wajuzi mambo kwenye mitandao ya kijamii kuwa huenda msanii huyo amerudia na mpenzi wake mwanadada King Alami.

Kupitia ukurasa wake wa instagram Noti Flow amepost picha ya King Alami akiwa amechora tattoo ya uso wake yenye caption inayosomeka kuwa “Alifanya mwenyewe,sijemuomba wala kumlipa”

Itakumbuka mapema mwezi Julai mwaka huu Noti Flow alithibitisha kuachana na mpenzi wake mwanadada King lami baada ya kudumu kwenye mahusiano kwa kipindi cha miezi mitatu.

Hitmaker huyo wa “Foto moto” alienda mbali zaidi na kusema kwamba alichukua maamuzi ya kuachana na mpenzi wake huyo kutokana na tabia ya usumbufu ambayo alikuwa nayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *